WAENDELEE ni asasi isiyo ya kiserikali iliyopo Mkoani Singida ambayo inawezesha shughuli za mbalimbali na miradi ya kuboresha kipato cha jamii katika Wilaya ya Singida ikiwemo kata za Mrama, Mtinko na Ngimu zilizopo Wilayani Singida.
Asasi hii inayojulikana kwa kifupi kama WAENDELEE, ilisajiliwa rasmi tarehe 26/08/2016 na kwa usajili namba S.A. 20805. Lengo la Taasisi hii ni kuibua na kuzitumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ndani na nje ya Nchi katika Nyanja za Mazingira, Elimu, Afya na Maji kwa manufaa ya wananchi waishio katika Mkoa wa Singida hususani Wilaya ya Singida ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa maendeleo endelevu.
Wajibu wa Asasi ya WAENDELEE katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira ni kutoa elimu kwa jamii, Kutafuta wafadhili mbalimbali wa kusaidia kuboresha na kuhifadhi mazingira na kutoa vifaa au vitendea kazi vya kusaidia uboreshaji wa mazingira kama vile nyenzo zaa kuoteshea miti.

